Mhe. Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela Mkoani Rukwa, aipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga kwa mafanikio mazuri ya uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga kwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 54.72 Kama chanzo mbadala cha fedha za kutekeleza miradi ya kuboresha huduma na Usafi wa Mazingira Tanga.
“Kipekee niwapongeze wadau wakubwa na wa muhimu waliofanikisha upatikanaji wa fedha hizi ambao ni Wizara ya Fedha, UNCDF, CMSA, DSE na NBC kwani wamekuwa mchango mkubwa sana katika kufanikisha jambo hili na hii ni Game changer katika sekta ya maji Nchini, hivyo nashauri Mamlaka nyingine kubwa nchini ziige mfano huu ili kuweza kujipatia fedha kuliko kutegemea kupata fedha kutoka katika mfuko wa maji.” alisema Mhe. Sangu.
Mhe. Sangu ameyasema hayo leo wakati wa kipindi cha mjadala na michango kutoka kwa wabunge baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Maji katika kikao cha 22 cha Bunge la Bajeti.