Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage amemwambia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kumwandalia zuria kwenye banda la maonesho ili aende akatoe elimu ya kukabiliana sekta ya uwekezaji katika sekta ya nyama.
Mwijage amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyoomba kiasi cha Shilingi 295,920,933,000. kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
“Sekta ya nyama inaweza kutuingizia dola bilioni 5 na kama kuna mtaalamu hapa anamashaka twende kwenye banda nimuoneshe kwa mahesabu huewezi kuwa na ng’ombe 35 milioni halafu ukashindwa kuuza nyama inayofikia bilioni sita kwa mwaka hata wale ng’ombe ungewachinja kwa miaka 10 niwekeeni zuria kwenye banda ya maonesho nije niwaoneshe” Mbunge Mwijage