Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesema kuwa imepokea ushauri uliotolewa na Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Peter Cherehani aliyeomba kuondolewa kwa makato makubwa kwa wakulima wa zao la Tumbaku yanayotokana na upandaji wa miche ya miti ambapo kwa bei ya sasa ni zaidi ya sh 813 kwa kila mche mmoja.
Akijibu swali hilo bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa “Tumepokea ushauri wa Mhe. Mbunge na tutakaa kikao na wadau kuweza kukubaliana kwa pamoja, kwahiyo tumechukua ushauri”.