Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Jacqueline Kainja amekabidhi viti 700 katika Wilaya saba za Mkoa huo kama mradi wa Wanawake wa UWT Mkoa wa Tabora na pia ametoa pesa Taslimu Tsh. milioni saba kuendeleza nyumba za Makatibu wa UWT Wilaya saba za Mkoa wa Tabora.
Akiongea baada ya kukabidhi vitu hivyo, Kainja amesema “Nitakabidhi kila Wilaya Tsh. milioni moja nikiamini kwenye ujenzi kuna sehemu tutafika, kwasababu nimesikia kuna wengine wana mchanga wengine wanaenda kupiga bati basi watawalipa Mafundi wakati huo tunaendelea kuvumiliana tunajikusanya huku na huku na mambo mengine yanaenda”
“Kuhusu miradi ya Wilaya leo kila Wilaya nitatoa viti 100, nimekuwa nikisimamia Mabaraza ya Wilaya kama nilivyosimamia Baraza la Mkoa lakimi unapofika kwenye kupanga mapambo viti tunakodi, kwahiyo naamini viti hivi mtakodisha na mtapata fedha za kufanya vitu vingine”