Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara akichangia makadirio ya Mapato na matumizi ya wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum ameiomba serikali kuandaa mjadala wa kitaifa wa kukomesha Ulawiti na ndoa za Jinsia moja ili kulinda mila na destuli za mtanzania.
Waitara amesema hayo bungeni jijini Dodoma ambapo ameoneshwa kushangazwa na Hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kutozungumzia kukomesha ulawiti na tamaduni ya ndoa ya jinsia moja wakati serikali imefanikiwa kuandaa kitabu cha kukomesha ukeketeji.
“Mwakyembe na mwenzake wametangaza hadharani wanatuonesha ndoa za wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake wewe hauoneshi hapa kuwa ni shida ya Taifa nimesikiliza ‘clip’ mama anasema hapewi ushirikiano halafu mwalimu amelawiti mtoto wa mtu,mama anamtoto wa kwanza wa kiume anamtegemea anauza mandazi anasomewsha mtoto analawitiwa shuleni halafu Waziri huwezi kusema hapaa hiyo haikubaliki watanzania wamechukia sana ushoga,hebu niangalie ya mimi ‘jayanti’ wa kikurwa CHIEF niolewe yaani nifungishwe ndoa na mwanaume mwenzangu au namtoto wangu napambana hapa namsomesa halafu nimkute mwalimu kamlawiti HAKI YA MUNGU AMA ZANGU AMA ZAKE” Mwita Waitara mbunge wa Tarime Vijijini