Mbunifu wa mavazi wa kiume Mtani amechaguliwa na Moet Chandon nakupelekwa Epernay nchini Ufaransa , kujifunza zaidi kuhusu Moet na Jinsi wanavyotunza mazingira na pia wamempa fursa nyingi ikiwa kukutana na wabunifu tofauti kutoka nji mbali mbali .
Mbunifu huyo alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, akiwa na afisa maendeleo ya biashara, Charles de Ponteves d’Amirat wa kinywaji hicho Afrika Mashariki, katika Hoteli ya Hyaat Regency, iliyopo Posta Jijini Dar, kuwa ameweza kujifunza mambo mengi ambayo hakuwa kuyajua huko nyuma na kuishukuru kampuni hiyo kwa kuwachukua wabunifu mbalimbali waweze kujifunza mambo mengi zaidi.
Mbunifu huyo wa mavazi ya kiume Bongo, anawavalisha suti mastaa wengi hapa Bongo, ameishukuru kampuni ya moetchandon kwa kumpeleka Epernay nchini Ufaransa, kwenye mahandaki maalum ya kusindikia kinywaji hicho ambapo kwenye shimo hilo miaka ya nyuma kipindi cha Vita ya dunia ya pili ya dunia walikuwa wakitoa msaada wa kuhifadhi watu na familia zao ndani ya shimo hilo.