Shankar Das, (46), ambaye ni mfugaji wa wanyama kutoka nchini India hivi karibuni alipigwa na butwaa baada ya mbuzi wake mmoja kuzaa kiumbe kisicho cha kawaida chenye sura inayofanana na binadamu.
Shankar alisema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa hai lakini cha kusikitisha alikufa baadaye. Pia inaaminika kuwa mtoto huyo wa mbuzi alifariki kutokana na mwonekano wake usio wa kawaida ambao ulionyesha kuwa hajakomaa kikamilifu.
Nchini India, kuzaliwa kwa mnyama mwenye ulemavu kunachukuliwa kuwa ishara mbaya au bahati mbaya pamoja na kukitihiri kwa maovu.