Mtu wangu wa nguvu, najua ushapita au kuishi mitaa yenye Mbwa wengi wakali na wapole, au pia unafuga Mbwa kwa ajili ya kukuhakikishia ulinzi nyumbani kwako, sasa leo nimeipata hii kutokea Kenya. Kituo cha TV cha K24 wameripoti kuhusu kero ya kelele za Mbwa kubweka kiholela imesababisha kutungwa kwa sheria ya kudhibiti ubwekaji wa aina hiyo.
Jiji la Nairobi limeingia tena kwenye headlines mpya baada ya kupitisha sheria itakayowabana wafugaji wa Mbwa. Ripoti zinasema iwapo Mbwa wako atabweka kwa dakika 6 mfululizo ndani ya saa moja au dakika tatu mfululizo ndani ya dakika 30 utatozwa faini ya Shilingi elfu tano za Kenya ambazo ni sawa na Shilingi laki moja na elfu saba mia sita za Tanzania au utatumikia kifungo cha miezi miwili jela.
Wataalamu wa mifugo wanasema pamoja na kupitishwa kwa sheria hiyo, kuna muda ukifika inakua vigumu sana kumfundisha Mbwa kubweka na kunyamaza.
>>>Kusema utamtrain mbwa, utajaribu kufanya hivyo na kumforce ila unakuwa unawapatia nafasi wezi, wezi watakuwa wanatime kuwa atabweka dakika sita halafu atanyamaza na wataingia ndani kufanya tukio:- Mtaalamu wa Mbwa.
ULIKOSA HII YA JACQUELINE MENGI KATULETEA BIASHARA YA FURNITURES UBUNIFU WAKE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI