Kutokana na uzoefu wake Mbwana Samatta ameunga mkono klabu za Ligi kuu bara ziruhusiwe kusajili wachezaji watano kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuleta ushindani na mafanikio ya timu.
Samatta anakipiga klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wamekuwa wanafanya vizuri kwenye mashindano ya ndani ya nchi na kimataifa amesema unaweza kuwa na wachezaji wengi kutoka nje ya nchi wakawa hawana faida kwani sehemu kubwa wanaocheza na kufanya vizuri wanakuwa ni wazawa na mfano ni klabu yake ya TP Mazembe.
Ameliambia Mwanaspoti kuwa “nafikiri uwepo wa wachezaji watano kutoka nje ya nchi ni nzuri kwa sababu ya ushindani wa wachezaji wenyewe kwa wenyewe na kwa timu na timu na ligi bora ni ile yenye mchanganyiko wa wachezaji, ligi inahitaji mseto wa wachezaji kutoka nje ya nchi lakini timu inahitaji wachezaji wazuri bila kujali ni kutoka nje ya nchi au wazawa, muhimu ni kiwango’
“Lakini pia unaweza kusajili wachezaji wengi wa kimataifa wakawa hawana faida na timu namaanisha viwango vyao vinakuwa chini zaidi ya wazawa waliopo na mfano hapa kwetu, wapo wengi lakini wanaocheza ni wachache”
Source:Mwanaspoti
Unapenda chochote kinachonifikia kisikupite? jiunge na mimi twitter kwa kubonyeza HAPA pia facebook na Instagram kwa kubonyeza FB na INSTA ili nikutumie kila kitu, kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi.