Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema Wananchi wote waliohusika kuushambulia kwa mawe Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela Claudia Kitta na timu nzima ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo watachukuliwa hatua kali kwani walidhamiria kuwaua Viongozi hao.
“Ni mkong’oto usiku kucha, sababu walirusha mawe na walidhamiria kumuua Mkuu wa Wilaya hawa wamechagua kuuawa wao, hili sio kinyume cha Haki ya Binadamu, haki ya binadamu alipaswa kuwa nayo yeye kabla hajampiga au hajaharibu lile gari” RC Mbeya
“Kikosi kazi kisitoke mpaka nione furaha imejaa moyoni, nawaambia ukweli na hapa bado sijakunjua kikosi kingine, hapa Mbeya kuna kikosi kipo Itende vimenyamaza, tunasubiri watu wajikunjue tupige king’ora cha mwisho” RC Mbeya