Kero nyingi wanazokumbanazo watu wengi walio kwenye Miji inayoendelea hapa Tanzania ni makazi holela na foleni kubwa katikati ya Miji hali inayopelekea kuchelewa kazini na mambo mengine,
Moja ya Jiji lenye changamoto hizo ni Jiji la Nbeya ambalo asilimia 70 ya makazi yamejengwa kiholela bila kufuata utaratibu wa kupimwa na mji kutokaa katika vipimo vinavyoendana na hali ya sasa.
Hali hiyo imesababisha Halmaashauri ya Jiji la Mbeya kutafuta Kampuni ya kupima Jiji zima na kuweka Mipango Mji na kurahisisha utoaji huduma na kuondoa foleni kwa ujumla.
AyoTV imempata Kiongozi wa Kampuni ambayo itafanya kazi ya kutengeneza Mbeya City Master Plan ya miaka 20 ijayo kuanzia mwaka 2019 mpaka 2039 atueleze wanampango gani na Jiji la Mbeya.
DC ACHARUKA MIRADI ZAIDI YA 100 KUTOPIMWA NA INJINIA “TUGAWANE MSHAHARA”