Kufuatia uwepo wa Nyoka aina ya Chatu kwenye Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilayani Chato Mkoani Geita ambaye baadhi ya wananchi kutoka maeneo tofauti walifika kwa lengo la kumwabudu Nyoka huyo kwa madai ni nyoka wa Baraka,Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Nchini imemchukua nyoka huyo na kufanikiwa kumpeleka Poli la akiba la Kigosi lililopo Wilayani Kahama kwaajili ya Hifadhi.
Nyoka huyo ambaye amechukua takribani siku 15 , huku akikusanya watu kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya Mkoa wa Geita, kwa madai ni nyoka wa maajabu kutokea kwenye kijiji hicho kwa sasa, ameondolewa na maafisa wanyamapori wakishirikiana na wataalum wa Nyoka kutoka Makumbusho ya Bujora Jijini Mwanza.