Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kupitia kampuni yake ya ujenzi na ushauri MCB inaendelea kusimamia miradi ipasavyo. Katika kutekeleza hayo, mapema hivi leo jengo la wizara ya Maliasili na Utalii lilipo Dodoma limekabidhiwa rasmi kwa Katibu wa wizara hiyo dkt. Hassan Abbas.
Awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la ghorofa tano kwa ajili ya ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii umekamilika, ambapo bilioni 17.2 zimetumika katika ujenzi huo.
Mkandarasi na Mshauri elekezi MCB wamekabidhi jengo hilo kwa wizara ili lianze kutumika.
Akiwakilisha taarifa ya ujenzi huo Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Tecknolojia Mbeya (MUST) prof. Aloys Mvuma amesema jengo hilo liko tayari kwa matumizi baada ya kukamilika september mwaka huu, pia ameipongeza serikali kwa kutoa fedha za ujenzi kwa wakati.
Nae Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii amewashukuru mkandarasi na mshauri elekezi kwa kazi nzuri na kuhakikisha jengo limekamilika kwa wakati,ambapo wizara hiyo ni ya kwanza kukamilisha ujenzi huo ulioanza mwishoni mwa mwaka 2021.
Kwa mujibu wa maelekezo ya waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa,kila wizara inapaswa kuhamia katika majengo yao ifikapo Januari 2024.