Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REA‘ Lutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo >>> ‘REA haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya fedha zote tunazofanyia kazi na hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’
>>>’Shughuli za REA haziwezi kusimama naserikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’ – Mwakahesya.
Ulikosa video ya kilichomchekesha Rais Magufuli japokuwa alikua kavaa sura ya kazi IKULU,? Tazama Video hii hapa chini
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE