Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Derick Dambuve (26), mkazi wa kijiji cha Mgoma wilayani Ngara kwa tuhuma za kuwaua mama na mtoto wake (2), baada ya mtuhumiwa kumfumania mwanamke huyo akifanya tendo la ndoa na Kajere Ibrahim (mchepuko mwingine) nyumbani kwa Derick.
“Huyu mama alitoroka nyumbani kwa mume wake kijiji cha Muruvangira na kwenda kijiji cha Mgoma anakoishi mtuhumiwa, kulikuwa na gulio akaamua kwenda baa na ndipo akakutana na mtuhumiwa akamtongoza wakakubaliana wakaanza kunywa pombe” RPC Kagera
“Mtuhumiwa ni fundi ujenzi na alikuwa na kazi hajamalizia, akamuomba rafiki yake amsaidie kumpeleka huyo hawara yake nyumbani,” RPC Kagera