Salma Ramadhan (34) Mama wa watoto wawili mkazi wa mtaa wa silvini malimbe Mwanza, amejikutana anaingia kwenye mgogoro na wapangaji wake kwa madai kuwa wapangaji hao wanamrubuni mwanae umri (14) mwanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza kujihusisha na mahusinano na mwanaume mwenye mahusiano na Mama yake, Kitendo ambacho Mama mwenye nyumba anadai kimepeleke mwanae kufanyiwa ukatili wa kubakwa na mchepuko wake huku akianza kuwindwa ili auwawe.
Salma amevunjika mkono kwa kile anachodai walimshawishi binti yake kumwaga sababu na mafuta sakafuni kitendo ambacho kilipelekea kudondoka na kuvunjika mkono.
Ayo TV, millardayo.com imefika nyumbani kwa Mama huyo na kufanya nae mahojiano amefunguka mengi kuhusu Mwanae kudaiwa kubwaka na mchepuko wake, Kuwindwa ili auwawe pamoja na chanzo cha mgogoro na Wapangaji wake.