Kumekuwa na vitendo kadhaa vya kuwatilia mashaka wanamichezo wa kike hasa pale wanapokuwa na uwezo mkubwa kuliko kawaida na mashaka zaidi hutiliwa kwenye uhalisia wa jinsi zao ambapo wengi huhofiwa kuwa si wanawake halisi bali ni wanaume .
Hii iliwahi kumkuta mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya na safari hii imemkuta mwanasoka toka Nigeria Genoveva Anonma ambaye katika hali ya kuhuzunisha alidhaniwa kuwa mwanaume .
Mbaya zaidi ni kwamba Genoveva alikutana na kadhia hii toka kwa Waafrika wenzie ambao ni viongozi wa mamlaka kuu za soka Afrika ambao walidhani binti huyu anadanganya kuhusu jinsia yake ya kike .
Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa ili kuthibitisha kuwa ni msichana na si mvulana kama ilivyokuwa inahofiwa nah ii ni kutokana na nguvu ambazo anazo akiwa uwanjani na ubora alioonyesha .
Genoveva akizungumza na vyombo vya habari alisema kuwa alidhani kuwa uthibitisho wa insi hufanywa hospitalini na alidhani angeitwa hospitalini lakini cha kushangaza ni kwamba alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa jambo ambalo anakiri kuwa lilimsababishia fedheha na hasira.
Kashfa hii ilianzishw akwenye muichuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kina mama ambapo viongozi wa Ghana , Nigeria na Afrika Kusini walizusha hoja kuwa wachezjai watatu wa Equatorial Guinea ni wanaume na si wanawake .
Hofu hii iliondolewa baada ya wachezaji hawa kiukaguliwa na kugundulika kuwa wanawake halisi .