Beki wa zamani wa Brazil Anderson Polga alikamatwa siku ya Jumatano kwa madai ya kushindwa kulipa malipo ya watoto.
Polisi wa Rio Grande do Sul walisema Polga mwenye umri wa miaka 44 alipelekwa jela nje ya mji wa Porto Alegre baada ya hakimu kuamuru akamatwe huku kiasi kinachodaiwa hakikufichuliwa.
Mawakili wa Polga hawakujibu ombi la maoni kutoka kwa The Associated Press.
Polga alikuwa mshiriki wa kikosi cha Brazil kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka wa 2002. Alicheza katika mechi mbili wakati wa mashindano.
Beki huyo alicheza Sporting Lisbon kwa takriban miaka tisa na alistaafu mwaka 2012 kama mchezaji wa Corinthians. Alichezea Gremio kati ya 1999 na 2003.