Mchina mmoja hivi karibuni alipoteza maisha alipokuwa akifanya mazoezi ya aina ya utata ambayo yanawahitaji wanaofanya zoezi hilo kuning’inia kwa kidevu pekee ili kupunguza maumivu ya shingo na uti wa mgongo kwa kupunguza shinikizo kwenye mishipa ya fahamu.
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, aina ya mazoezi ya ajabu imekuwa ikivutia kote nchini China.
Kimsingi inahusisha namna ya kunyumbulisha mwili wa mtu huku ukining’inia hewani ukiwa umetumia kamba ya ngozi kwenye kidevu.
Inasemekana kwamba ilivumbuliwa mwaka wa 2017 na mzaliwa wa Shenyang, Sun Rongchun kama njia ya kupunguza maumivu ya mgongo, mabadiliko ya shingo yalianza kuonekana katika bustani na ukumbi wa michezo wa nje kote nchini.
Ingawa kuning’inia hewani kwa kidevu haionekani kuwa kitu salama zaidi ulimwenguni, wataalam wanasema sio sahihi kiafya japo wanadai hufanya maajabu na uponyaji kwa maumivu ya shingo na mgongo.
Bado, madaktari wamekuwa wakionya juu ya hatari ya mazoezi haya hatari kwa miaka mingi na mkasa wa hivi karibuni unaonyesha kwamba inapofanywa vibaya, aina hii ya mazoezi inaweza kuwa mbaya hata kusababisha kifo.