Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara, inamshikilia Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT- Usharika wa Ufana, Emanuel Petro Guse kwa kuendesha mikopo umiza bila ya leseni ya biashara ya ukopeshaji fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa huo Holle Makungu amesema kuwa hapo awali walipokea malalamiko kutoka kwa mwananchi wa Bashneti aliyekopa kwa Mchungaji huyo kiasi cha Shilingi Laki Mbili na kurejesha kiasi cha Shilingi Laki Nne.
Makungu ameongeza kuwa mara baada ya kubaini hilo waliamua kumuita Mchungaji Guse ambaye alikaidi wito huo na baadaye TAKUKURU iliamua kutuma makachero wake kwenda kumkamata na hata baada ya kumhoji kama anafanya biashara hiyo Mchungaji huyo alikataa na walipoamua kufanya ukaguzi ndani ya nyumba yake walikutana na mikataba 48 ya mikopo umiza.
Aidha TAKUKURU mkoani humo, imetoa wito kwa wananchi wote walioathirika na mikopo umiza ya mchungaji huyo, waweze kufika ofisini hapo ili changamoto zao ziweze kushughulikiwa kwa pamoja.
MKE WA TUNDU LISSU AZUNGUMZA MBELE YA WAFUASI WA CHADEMA MBAGALA