Msemaji wa Serikali Dr. Hassan Abbas amekanusha taarifa zilizotolewa kuhusu mfanyabiashara aliyedai kakatazwa kuuza sukari Tanzania bara ambapo amemtaka muwekezaji wa kiwanda cha sukari cha Zanzibar Sugar Factory Ltd kuhakikisha anakidhi mahitaji ya bidhaa hiyo kwani sukari yake inahitajika zaidi Zanzibar ambako bado hajakidhi mahitaji.
Ameongeza Tanzania Bara huzalisha tani 306,226 kwa matumizi ya kawaida ambapo hadi kufikia March 2018, kulikuwa na nakisi laki moja na thelathini kwa matumizi ya kawaida kutokana na hali hiyo serikali imeridhia kutoa vibali kwa kampuni nne kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya msimu 2017-2018.
Waziri Jafo baada ya kukuta wananchi wamechanga Milioni 26 kujenga kituo cha afya