Wakati mazishi ya Mwanahabari na Mtangazaji maarufu Fred Fidelis Masawe ‘Fredwaa’ yakiwa yamefanyika Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro aliyefariki kwa ajali ya gari maeneo ya Kawe DSM, Dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo Condrad Fidelis mdogo wa Fredwaa amesema sababu iliyopelekea ajali hiyo ni wakati wanajiandaa kuli-over take gari waliingia pembeni ya barabara wakati wakitoka kwenye biashara zao
“Kilichotokea ni ajali ya Gari na tulipokuwa tunataka kujiokoa tukaingia kwenye sewerage system ya barabara hali iliyopelekea mwenzangu kupata mshtuko mkubwa na mimi ndio nilikuwa naendesha tukaingiliwa mbele na gari”-Condrad Fidelisi Masawe.