Rapa wa Marekani Meek Mill amesema huenda akahamia Dubai, Falme za Kiarabu, kwa nia ya kuacha kuvuta sigara.
Meek Mill alisema aligundulika kuwa na emphysema, na akashauriwa na daktari wake kuacha kuvuta sigara ili kuepuka kukatisha maisha yake.
Alisema hayo alipokuwa akijibu habari za mfanyakazi mwenzake, Snoop Dogg kuacha kuvuta sigara.
Kwenye ukurasa wake wa X, Mill aliandika, “Ninaenda Dubai na kuacha kabisa kuvuta sigara… Nikimfuata Snoop, daktari wangu alisema nilipata ugonjwa wa emphysema ikiwa sitaacha kuvuta sigara na utapunguza nusu ya maisha yangu.
“Nilikuwa mraibu wa nikotini na bangi ililikuwa na kemikali nyingi na hatari sana kucheza na akili yangu!”