February 16 2016 Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako aliwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa juu wa Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutokana na kutotekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika taasisi zilizo chini ya Wizara na pia kupisha uchunguzi zaidi kutokana na taarifa ya mkaguzi mkuu wa ndani wa Serikali.
Baada ya Wizara ya Elimu kumuagiza mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali kufanya uchunguzi bodi ya mikopo ya elimu ya juu, wizara imepokea taarifa ya uchunguzi huo.
June 15 2016 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako ameisoma taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema kuwa wamebaini kuwa kuna udhaifu katika ufuatiliaji wa urejeshaji na katika mfumo wa utunzaji taarifa za marejesho.
Kutokana na matokeo ya uchunguzi huo serikali imetoa wiki mbili kwa bodi ya mikopo kupitia dosari zote na kuwapatia mashtaka ya kujibu watumishi waliosimamishwa kazi na kuunganisha mfumo wa utoaji mikopo na urejeshaji mara moja.
ULIKOSA HII WAZIRI WA ELIMU KUWAONDOA WANNE KAZINI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE