Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, amesema ameiona barua ya wazi ya Baba Askofu Mwamakula ya kumtaka amsamehe Mhariri wa Tanzanite Cyprian Musiba anayemdai Tsh.Bilioni 9 kwa tuhuma za kumchafua lakini amesema hawezi kumsamehe.
Kupitia majibu yake hayo Membe amesema “Baba Askofu Salaam na Asante kwa barua yako ambayo umenitaka nimsamehe Musiba kwasababu amesalimu amri na kwamba hana hela hata kama atauza Kijiji, Baba Askofu, sababu ulizozitoa hazina mashiko kwa sababu Musiba hajaniomba radhi, hajasalimu amri na amechelewa! aidha hata kama hana hela kama unavyosema, anazo mali zisizohamishika na hizo zote zitapigwa mnada”- Bernard Membe
Unaweza ukabonyeza play kufahamu stori kamili.