Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Bernard Membe amehojiwa kwa saa tano na kamati ya maadili ya CCM mjini Dodoma, kubainisha kuwa mahojiano hayo yamemuacha na furaha ya ajabu.
“Tulikuwa na mkutano wa masaa matano ya mijadala mikubwa ya kitaifa inayohusu Chama chetu (CCM) na nimekuwa mtu wa furaha ajabu kwasababu nimepata nafasi nzuri ya kujadili masuala ya kitaifa na kimataifa, nimepata nafasi nzuri ya kufafanua mambo kadhaa ambayo Chama walitaka kuyajua” – Bernard Membe
“Sasa hivi mimi na Mke wangu tunaenda kula chakula katika Hotel ambayo haijulikani, lakini niwaambie safari hii ya kuja Dodoma ilikuwa ni manufaa makubwa sana kwangu, kwa Chama na kwa Taifa letu, mengine yatakuwa yanapatikana kidogokidogo nikishiba”-Membe
MAAGIZO YA KAMISHNA MPYA ZIMAMOTO “ASKARI WAZEMBE TUTAWAFUKUZA”