Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya stori kubwa ni hii ya gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Wanaume wenye korodani zisizoshuka hatarini’, Gazeti hilo limeripoti kuwa wanaume ambao korodani zao hazijashuka kwenye mfuko wake wapo hatarini kwani kuna uwezekano mkubwa wa kugeuka kuwa saratani zikiwa tumboni.
Gazeti hilo lilifanya mahojiano na Daktari Bingwa wa Mfumo wa Njia ya Mkojo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ‘MNH’ Ryuba Nyamsogoro ambapo aliyazungumza haya………
>>>’kawaida mwanaume ana korodani mbili, moja ikiwa upande wa kushoto na nyingine upande wake wa kulia. Huwa zinatengenezewa tumboni na baadae hushuka hadi katika vifuko vyake vilivyoko nje ya mwili wa mwanaume karibu na uume‘
#MTANZANIA Wanaume ambao korodani zao hazijashuka kwenye mfuko wake wapo hatarini kupata saratani zikiwa tumboni pic.twitter.com/ZB8f7z7gx9
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
Daktari alieleza sababu mbalimbali ambazo huweza kuchangia hali hiyo ikiwamo mtoto kuzaliwa akiwa hajatimiza muda wake (njiti), pacha au kuzaliwa akiwa na upungufu wa homoni ya androgen.
Daktari huyo aliongeza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa katika vizazi hai 100 vya watoto wa kiume kila mwaka ulimwenguni wanne huzaliwa wakiwa na tatizo hilo.
>>>’Kwa hapa nchini bado hatuna takwimu halisi za hali ilivyo lakini hapa muhimbili tumekua tukipokea takribani watoto wanne wenye tatizo la korodani kutoshuka na kuwafanyia upasuaji’ :- Daktari
#HabariLEO Waziri Mkuu Majaliwa abaini changamoto mabasi ya haraka, asema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea pic.twitter.com/Hvv2bwVkKP
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#NIPASHE Tanesco imepunguza wizi wa nishati ya umeme kwa 6% ktk miaka sita iliyopita. pic.twitter.com/CH4UpirhBh
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#MWANANCHI Udart inatarajia kuanza kuuza hisa zake ili kuwapa fursa wananchi wengi kumiliki kampuni hiyo pic.twitter.com/NZSJz9PMDR
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#MTANZANIA Serikali imefuta mchakato wa ada elekezi kwa ajili ya shule za msingi na sekondari za binafsi pic.twitter.com/KyMyX14fpS
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#MAJIRA Waziri Mkuu Majaliwa awataka wakazi wa Kimara, K'ndoni, Morocco kutumia mabasi ya haraka kupunguza foleni pic.twitter.com/Rm3JXiboaF
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#MWANANCHI Kundi linalovamia makazi usiku na kubaka wanawake laibuka Kigoma, polisi yamkamata mmoja pic.twitter.com/HeVastM1Ss
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#MWANANCHI Polisi Z'bar imeahirisha kumhoji Maalim Seif kwa sababu zilizoelezwa kuwa nje ya uwezo wa jeshi hilo pic.twitter.com/kJjQrYNDlf
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#MWANANCHI Mkazi Bangkok Thailand ang'atwa uume na chatu akiwa chooni, apambana kwa dk kadhaa kabla ya kupata msaada pic.twitter.com/IgwtNBlewy
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#JamboLEO Utafiti Repoa umebaini walimu wengi nchini wana uelewa mdogo wakilinganishwa na wenzao Afrika Mashariki pic.twitter.com/uWS1IGsp9E
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
#NIPASHE Watatu Katavi mbaroni kwa kukutwa na kadi 19 za watu tofauti ambazo tayari walishazitumia kutoa mil 3.68 pic.twitter.com/UpF11WsJF2
— millardayo (@millardayo) May 28, 2016
UNAWEZA KUANGALIA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA MAY 28 2016 KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE