Logistic meneja wa msanii Davido, Israel Afeare, maarufu kama Israel DMW, ameomba radhi kwa jamii ya Waislamu kutokana na video hiyo yenye utata iliyopostiwa na boss wake.
Kumbuka kwamba Davido alikumbwa na mzozo baada ya kupost video ya wimbo mpya wa Logos Olori, iliyoonyesha watu waliokuwa wakisali kwa njia ya Kiislamu na kucheza wimbo huo msikitini hata hivyo baada ya makasiriko ya umma na comment kibao Davido,, alifuta video hiyo bila kuomba radhi.
Baada ya kilio cha umma,na jamii ya Waislamu bado inadai msamaha wa umma kutoka kwa Davido mwenyewe.
Akijibu kuhusu tukio hilo, Israel DMW, katika chapisho kwenye Instagram story yake siku ya Jumatano, aliomba msamaha kwa niaba ya Davido.
Israel ilitoa wito kwa Waislamu, akisema kuwa video hiyo ni juhudi ya burudani ambayo iliwasilishwa kimakosa.
Alisema, “Wacha niwaombe radhi haswa ndugu na dada zangu Waislamu, kwenye video ambayo ilipostiwa na kuvunja maadili ya kidini
“Ilikuwa ni juhudi ya burudani iliyowasilishwa kimakosa. Nawapenda wote.”
“It was purely an entertainment effort wrongly presented. Make una no vex. Love you all.”