Lionel Messi amekanusha madai kwamba alizungumza na rais wa Barcelona Joan Laporta baada ya hafla ya Jumatatu ya tuzo ya Ballon d’Or Gala mjini Paris.
Kulingana na podikasti “Jijantes FC,” Messi na Laporta walizungumza na kukubaliana kukutana wakati fulani kutafuta tarehe bora zaidi ya mchezo wa kuaga Messi huko Barcelona.
Lakini Messi alikanusha vikali na kuandika kwenye mtandao wa kijamii: “Unadanganya… kwa mara nyingine tena…”
Mwandishi wa habari aliyehusika na story hiyo, Gerard Romero, alienda kwenye ukurasa wake wa X kuomba msamaha kwa makosa yake haraka baada ya kukataa kwa Messi. “naomba radhi mara elfumoja kwa wote, na ELFU ZAIDI.
Nimedanganywa tena na jambo linalohusiana na LEO. Sijifunzi. Samahani. VERY f***ed up. Ninakubali kila unachoniambia leo na Ninaahidi kwamba tutajitahidi kuhakikisha kwamba halijirudii tena,” aliandika.
Msimu wa Inter Miami ulimalizika mapema kutokana na kushindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano ya MLS, hivyo hatakuwa uwanjani hadi mechi ya Argentina ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay na Brazil mwezi ujao.