Argentina imemuita Lionel Messi kwa ajili ya mechi zijazo za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la Amerika Kusini licha ya yeye kuwa kwenye orodha ya majeruhi katika klabu yake ya Inter Miami.
Messi alikosa kichapo cha 4-1 cha Inter dhidi ya Chicago Jumatano huku akiendelea kutatizika na utimamu wake — ameichezea klabu hiyo kwa dakika 37 tu tangu Septemba 3.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amekosa mechi tatu zilizopita za Inter na tano kati ya sita zilizopita.
Argentina watakuwa wenyeji wa Paraguay mnamo Oktoba 12 na kisha kusafiri kucheza na Peru siku tano baadaye katika mechi za CONMEBOL za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026.
Mchezaji mwenzake wa Messi Miami, winga Facundo Farias mwenye umri wa miaka 21, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa mara ya kwanza.