Hali hiyo imetokana na mwenendo mbaya wa matokeo wanayopata kwa sasa hususan mechi nne mfululizo zilizopita baada ya kufungwa na Mgambo JKT bao 1-0, JKT Ruvu mabao 3-2 huku ikitoka sare na Mbeya City 1-1 na Tanzania Prisons 0-0.
Amezungumza na gazeti la Mwanaspoti na kusema kiungo huyu anatakiwa kuonyesha utofauti wake na wachezaji wengine ambao hawamo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania.
“Ninaamini washambuliaji wangu wote wangekuwa wanajituma na bidii kama Tambwe (Amissi) basi timu yangu isingekuwa inapata matokeo mabaya, ukiangalia mchezaji kama Messi ana heshima kubwa katika taifa, anaichezea timu ya taifa, hivyo anatakiwa kuonyesha utofauti wake na wachezaji wengine katika timu kwa kutoa msaada mkubwa katika timu kwa kufunga mabao.
“Yeye amefunga bao moja pekee katika mechi nane alizocheza za ligi, Tambwe amefunga tisa katika mechi nane alizocheza, hivyo Messi anahitaji kubadilika,”alisema Logarusic akionyesha kukerwa na kutojitambua kwa baadhi ya wachezaji.
Ingawa amekuwa mgumu kuzungumzia tuhuma hizo za kocha lakini Messi wiki iliyopita aliliambia Mwanaspoti kuwa kiwango chake bado kipo juu na hakijashuka, shutuma hizo ni kutokana hali iliyochafuka Simba kila mchezaji anaonekana hafai kutokana na presha.