Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza kukamatwa kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya kiwanja cha gofu cha klabu ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro na kuwekwa ndani kwa madai ya kutolipa Milioni 26 za kodi ya ardhi tangu mwaka 2013.
Pia, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingilia kati suala hilo ili wanachama wa klabu hiyo wapate haki zao.
“Nashangaa mpaka sasa mmiliki wa Moshi klabu hajakamatwa na kupelekwa mahakamani kwa kutolipa kodi ya ardhi kwa muda mrefu hadi kufikia Sh26 milioni,” Raibu.