Wakuu wa Shule za Sekondari na Maofisa elimu wa Kata zote za Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamelazimika kuchangishana vifaa mbalimbali vya kufundishia kwa ajili ya kuwezesha kufunguliwa Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Mwasekwa.
Shule hiyo ya Sekondari ya Mwansekwa ndiyo ambayo Rais Dk. John Magufuli wakati wa ziara yake Mkoani Mbeya mwezi April mwaka jana aliichangia Milioni kumi ili kukamilisha ujenzi wake.
Baada ya kukamilika ujenzi wa shule hiyo, ilikabiliwa na tatizo la ukosefu wa vifaa vya kufundishia wanafunzi, hali iliyosababisha ikwame kufunguliwa.
Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi, aliwashukuru Wakuu hao wa Shule za Sekondari kwa michango waliyoitoa kwenye shule hiyo.
Mwashilindi aliwataka wananchi wa Kata ya Mwansekwa kuhakikisha wanaitunza shule hiyo kwa kushiriki kuchanga michango mbalimbali kwa ajili ya kukarabati miundombinu.
SERIKALI YAWAONYA WAAJIRI WASIRITHISHA UJUZI KWA WAZAWA “KWA MUJIBU WA SHERIA”