Mfalme Charles III anatarajiwa kufanya ziara na mkewe, Malkia Camilla hadi Scotland, Ireland Kaskazini na Wales siku chache kabla ya mazishi ya mamake, Malkia Elizabeth Il Septemba 19.
Kituo cha kwanza kitakuwa Scotland, ambapo watatembelea bunge la Scotland na kujiunga na mkesha wa kumbukumbu ya mfalme.
Siku ya Jumanne, wanandoa wa kifalme watasafiri kwa ndege hadi Belfast na kutembelea Jumba la Hillsborough, ambapo watatazama maonyesho ya ushirika mrefu wa Malkia na Ireland ya Kaskazini.
Pia watahudhuria ibada ya kumbukumbu ya Malkia na kupokea ujumbe wa rambirambi wakiongozwa na spika wa Bunge la Ireland Kaskazini.
Baada ya kurejea London, ambako watashuhudia kuwasili kwa jeneza la Malkia Elizabeth II, wanandoa hao watasafiri hadi Wales siku ya ljumaa.