Mfalme wa Jordan Abdullah II ametangaza kutoa msaada wa dharura wa matibabu kwa Gaza Jumatatu, Novemba 6.
“Wanajeshi jasiri wa Jeshi la Wanahewa wameshusha kwa kutumia ndege msaada wa dharura wa matibabu katika hospitali huko Gaza usiku wa manane,” mfalme amesema kwenye X (zamani ikiitwa Twitter), kabla ya kuongeza: “Ni jukumu letu kusaidia kaka na dada zetu waliojeruhiwa katika vita dhidi ya Gaza. Daima tutakuwepo kwa ajili ya ndugu zetu wa Kipalestina.
Israel inasema vikosi vyake vimeigawanya Gaza mara mbili baada ya mashambulizi yake ya ardhini dhidi ya Hamas kufika katika pwani ya Mediterania katika ardhi ya Palestina. Msemaji wa jeshi alisema kuwa mji wa Gaza sasa umezingirwa kabisa.
Kumekuwa na mashambulizi ya angani na milipuko mikubwa kaskazini mwa eneo hilo – ambayo ni mikali zaidi tangu vita kuanza, mwandishi wa BBC katika Ukanda wa Gaza amesema. Huduma za simu na intaneti zimekatwa tena.
Umoja wa Mataifa – ambao ni makazi ya watu wengi wa Gazan milioni 1.5 waliotoroka makazi yao – unasema maeneo 48 ya Ukanda wa Gaza yameharibiwa tangu vita vilipoanza.