Mfanyabiashara mkubwa wa maduka na kiwanda cha Unga mkoani Kigoma Khalifan Mussa Kwagula(55) aliyekuwa amepotea kwa takribani siku tatu mwili wake umeopolewa na Jeshi la zimamoto na uokoji akiwa amekufa katika makutano ya Mto Luiche na Ziwa Tanganyika.
Ndugu wa marehemu ameeleza aliondoka nyumbani siku ya Alhamisi wiki hii majira ya sa nane usiku akiaga mke wake kuwa anaenda katika kiwanda cha unga moja ya sehemu ya baishara yake.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu Khalifan Mussa wanasema baada ya muda tangu alipoondoka nyumbani walikuta gari lake aina ya Landcruiser Toyota likiwa limepaki karibu na mto Luiche huku funguo ya gari na vitu vingine vikiwa ndani yake lakini ndugu yao hawakumukuta ndani ya gari hilo.
Mussa Madua mdogo wa marehemu anaeleza jitihada za kuendelea kumtafuta zilifanyika ikiwemo kupiga namba zake za simu ambazo inaelezwa kuwa hazikupatikana kwa kipindi chote.
Inspekta Jacob Chacha Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoji Mkoani Kigoma amesema marehemu mwenye umri wa miaka 55 mwili wake umeopolewa katika makutano ya ziwa Tanganyika na Mto Luiche.
“Mpaka sasa taarifa zipo mbalimbali ambazo hazijawa rasimi lakini uchunguzi unaendelea na kwa sasa swala hili tumeliacha kwa jeshi la polisi ili liweze kuendelea na taratibu zaidi cha chanjo harisi la tukio hili,mara baada ya chanzo kubainia hatua zingine zitafaatwa ikiwemo taarifa rasimi kuhusiana na mtu huyu aliypotea kwa muda wa siku tatu”–> Insp. Chacha