Mashahidi 24 kutoa ushahidi wa shambulio na kugaidi amri ya Wizara ya Madini dhidi ya Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti na Wafanyakazi wake sita waliosomewa maelezo yao ya awali leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara katika tukio lililotokea marchi 13 Mwaka huu katika mgodi uliopo kitalu B unaomilikiwa na kampuni ya Gem & Rock Venture.
Wakisomewa maelezo ya awali na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Mosses Hamilton Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Charles Uiso ilidaiwa kuwa katika kesi hiyo Serikali itawasilisha vielelezo 11 Enock Nanyaro.
Hamilton alidai katika kesi ya shambuli inawahusu washitakiwa sita akiwemo Petro Exsaud(48) mkazi wa Moshono Arusha, Mosses Kelerwa(45) mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya (44) mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses Sirikwa (46) Mkazi wa Ilboru, Dausen Mollel(58) Mkazi wa Ilboru na, Enock Nanyaro(32) mkazi wa Arusha kesi hiyo itakuwa na mashahidi 16 na vielelezo 6.
Mwendesha Mashitaka huyo alidai katika shitaka lingine la kukaidi amri ya Wizara linalomkabili Saitoti na Nanyaro litakuwa na mashahidi 8 na vielelezo 5 na mashahidi wanahifadhi hadi mei 10 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Katika maelezo ya awali ,Hamilton alidai kuwa March 13 mwaka huu wafanyakazi sita wa Gem & Rock Venture waliwashambulia kwa majabali na vifaa vya uchimbaji watumishi wa Taasisi za serikali na wafanyakazi sita wa Franone akiwemo Benson Banash,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbert Albogast,Mussa Unambe na Bonfance Mollel na kuwapatia majeraha makubwa usoni.
Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa Hilo wakati wakijua wazi kuwa kufanya kosa hilo nikosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana maelezo ya awali na dhamana yao iliendelea kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamini mmoja na Bondi ya shilingi milioni moja
Katika maelezo ya awali ya washitakiwa wawili Saitoti na Nanyaro Mwendesha Mashitaka Hamilton ilidaiwa wameshitakiwa kwa kwa shitaka moja la kukaidi amri ya Wizara ya Madini ya ambapo ilidaiwa kuwa walizuiwa kufanya shughuli za uchimbaji baada ya mtobozano na Kitalu C lakini walikaidi na kuendelea na kazi wakati wakijua wazi ni kosa kisheria kuzuia agizo la Serikali.
Washitakiwa walikana shitaka hilo na dhamana ya mtu mmoja mmoja iliendea na kesi ilihairishwa hadi mei 10 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa rasmi.