Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro imetoa uamuzi wa mapingamizi ya kesi iliyokuwa inamkabili Mkurugenzi wa kampuni ya Gem and rock ventures joel Saitoti Molele na kuwaachilia huru washitakiwa wote wawili huru
Akitoa uamuzi huo hakimu mfawidhi mkazi wa mahakama ya Simanjiro Daud Uiso amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo Kwa mjibu wa kifungu na 124 ya Sheria ya mwenendo wa Jinai , Sura ya 16 Kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 .
Mnamo tarehe 9/06/2023, wakili anayemtetea Joel Saitoti Mollel na Enock Benjamin Nanyoro alipeleka mapingamizi mawili ya kisheria Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro ya kwamba Mahakama ya Wilaya haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi ya Jinai Na 42 /2023 iliyofunguliwa na upande wa Jamhuri Kwa kosa la kutoheshimu Amri ya mkaguzi wa migodi iliyomtaka kuzuia shughuli zote za uchimbaji wa madini katika leseni ya madini Na PML 0040SMN mnamo tarehe 10.03.2023 katika Mgodi unaomilikiwa na Kampuni ya Gem and Rock Ventures Co Ltd na Mahakama ya Wilaya ilisikiliza mapingamizi hayo Kwa kuwasikiliza pande zote mbili.