Mahakama nchini Nigeria imemhukumu kifo mfanyabiashara wa China baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Ummu Kulthum Sani mwaka 2022.
Frank Geng Quarong alipatikana katika chumba chake baada ya kumchoma kisu mara kadhaa.
Mauaji ya mwanafunzi huyo wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 yalishtua Wanigeria na tukio hilo likafuatiliwa kwa karibu.
Hukumu za kifo ni nadra nchini Nigeria. Quarong ana siku 90 za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya familia, kaka wa mwathiriwa, Sadiq Sani, alielezea hukumu ya kifo kwa kunyongwa iliyotolewa na mahakama ya Kano kuwa ni haki. Alisema kuwa yeyote anayemuua yeyote anastahili kuuawa pia.
“Tunamshukuru Mungu kwa kutuonyesha siku hii… Naomba kwamba roho ya dada yangu iendelee kupumzika kwa amani,” aliambia BBC.
Familia yake inamkumbuka mwanafunzi huyo mchanga wa kilimo kama mkarimu na mcheshi.
Quarong, 49, na Bi Sani walikuwa kwenye uhusiano tangu 2020 baada ya kukutana katika duka kubwa, kulingana na Bw Sani.
Mfanyabiashara huyo alikuwa nchini humo akifanya kazi katika kampuni ya nguo ya Nigeria kwa mujibu wa BBC.