Mfanyabiashara wa Madini katika Soko la Dhahabu Mkoani Geita Fahad Mohamed anayemiriki Kampuni ya SAB- GOLD- LIMITED (SGL) inayofanya kazi ya Kununua Dhahabu Mkoani humo ametapeliwa kwa Njia ya Wizi kiasi cha Shilingi Milioni 115 na Kijana, Yotham Komba Mkazi wa Geita na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza kwa Masikitiko Makubwa Mfanyabiashara wa Madini Firoz Khan amesema Kijana huyo anayetuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo January 16 mwaka huu ambapo alifika Ofisini kwa Mfanyabiashara huyo na kuomba kiasi cha shilingi Milioni 115 akidai ataleta kiasi cha Dhahabu kilo moja ambapo baada ya hapo alitokomea kusikojulikana huku Begi la Fedha pamoja na Simu akizitelekeza.
“Alikuja kijana mmoja ambaye anatambulika kama Mmoja katika Mhudumu ama Mfanyakazi katika Ofisi za Dira humu na Kuja kujielezea kwamba ana dhahabu kilo moja hivyo akaomba pesa na Ofisi Sab Gold walimpa pesa kiasi cha Milioni 115 pesa za Kitanzania Taslimu at aliondoka nazo akiahidi kwamba anakuja na Dhahabu ya kilo Moja lakini Muda umepita , ” Mfanyabiashara Mohamed.
Khan amesema Wafanyabiashara wa dhahabu wamekuwa na Mtindo wa kupeana fedha huku wakiahidiana kupewa Mzigo wa Madini ambapo hata huyo kijana anayetuhumiwa amekuwa akifanya Biashara na Mfanyabiashara hiyo mara kadhaa ambapo kipindi hiki baada ya kukabidhiwa fedha hizo alitokomea na Mpaka sasa hajulikani aliko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko la Dhahabu Mkoa wa Geita George Maloba amekiri kuwepo kwa Matukio ya Udanganyifu katika soko hilo kwa kile kinachofanywa na Wafanyabiashara wa Madini ikiwemo kuaminiana kwa kukopeshana Fedha na Wanunuzi mbalimbali wa Madini ambao wamekuwa wakitokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP, Safia Jongo amethibitisha tukio hilo huku akisema amekuwa akipokea kesi nyingi hasa za wafanyabiashara wa Madini kudhulumiana na kutapeliana kwa njia ya wizi ambapo amewataka kuacha tabia ya kuaminiana na Badala yake watumie njia sahihi ya kununua Dhahabu kupitia dhamana walizonazo.
Sambamba na hilo ACP.Jongo amesema Matukio hayo yamekuwa ni chanzo cha Mauwaji ndani ya Mkoa wa Geita ambapo amewataka kuhakikisha wanapokuwa wanapeana fedha hizo wawe wanaandikishana kupitia Biashara wanazozifanya.