Mkuu wa Mkoa Mbeya Albert Chalamila amepita kila duka Kabwe stand kukusanya mifuko ya rambo (plastic) ambayo imepigwa marufuku kutumika kuanzia June 1, 2019 nchi nzima.
Mkuu wa Mkoa amesema watu wa Mbeya wanatakiwa kuona mifuko ya rambo kama bangi vile kwani vyote vimekatazwa kisheria na atakayekutwa nao atakutana na kifungo.