Familia ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini ambaye pia ndiye aliyelikomboa taifa hilo kutoka kwa ukoloni hayati Nelson Mandela, wamelaani vikali kitendo cha baadhi ya viongozi wa serikali kutumia vibaya Dola Milioni 22 sawa na Tshs Bil 56.2 zilizotolewa kwa ajili ya shughuli ya mazishi ya baba yao mwaka 2013.
Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Busisiwe Mkhwebane nchini humo, viongozi wa Jimbo la Cape Mashariki walizidisha kiwango hicho cha pesa kwenye bajeti halisi iliyotakiwa kumaliza shughuli nzima ya msiba kwa kuongeza gharama za vitu vilivyohitajika.
Mjukuu mkubwa wa Mandela ajulikanaye kama Mandla ameeleza jinsi gani familia yake imeumizwa na viogozi ambao walitumia kifo cha hayati Mandela kujinufaisha wenyewe, tena kwenye kipindi ambacho familia ilikuwa kwenye majonzi makubwa.
LIVE: Makamu wa Rais Samia Suluhu amehamia rasmi Dodoma