April 6 2016 Rais John Magufuli wa Tanzania aliungana na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika ufunguzi wa daraja la kimataifa mpakani mwa Tanzania na Rwanda na wakafungua pia Ofisi ya pamoja itakayokua inadili na ishu za uhamiaji upande wa Tanzania na Rwanda kwenye huo mpaka.
Kwenye nukuu zilizotolewa na ofisi ya Rais Rwanda kutoka kwa Rais Kagame ambaye aliyasema haya baada ya Rais Magufuli kuondoka Rwanda, ni pamoja na hii >>> ‘Kwa uongozi mpya, sasa Rwanda na Tanzania watafurahia uhusiano mzuri na kila tatizo litatuliwa‘
Hii ni kauli ambayo Rais Kagame aliisema wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda na aliyazungumza haya mbele ya maelfu ya Wananchi waliokusanyika kwenye uwanja wa mpira Amahoro Kigali Rwanda ambapo pia Rais Kagame alimshukuru Rais Magufuli kwa kuitembelea Rwanda kupitia page yake ya Twitter.
Rais Kagame alisisitiza pia kwamba ‘Wote wanaojaribu kuliangamiza taifa letu ikiwemo na wale wanaowatumia nchi ambazo ni jirani zetu kamwe hawatoweza kufanikiwa‘
What happened 22 years ago is never easy to comprehend but today Rwandans and other people of goodwill remember and honour lives lost
— Paul Kagame (@PaulKagame) April 7, 2016
.
We thank President @MagufuliJP for visiting to express solidarity with Rwandans and strengthen fraternal ties between #Tanzania & #Rwanda
— Paul Kagame (@PaulKagame) April 7, 2016
ULIIKOSA YA RAIS MAGUFULI ALIVYOTUA KWA NDEGE DSM AKITOKEA RWANDA? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
ULIIKOSA HII? KWANINI RAIS MAGUFULI HAPENDI KUSAFIRI NJE YA NCHI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE