Leo May 13, 2018 nakusogezea stori kutoka visiwani Zanzibar ambapo Serikali ya Zanzibar imeagiza zaidi ya waalimu 300 wa masomo ya Sayansi kutoka nchini Nigeria ambao tayari wameanza kuwasili visiwani humo.
Kwa mujibu wa serikali ya Zanzibar, waalimu hao wanaoingia kwa awamu wanatarajiwa kuziba pengo la uhitaji wa zaidi ya waalimu 300 wa masomo hayo ya Sayansi.
Waziri wa Elimu Zanzibar Mmanga Mjengo amesema ujio huo utasaidia kuamsha pia morali ya walimu wengine wa masomo ya sayansi visiwani humo.
Ameongeza pia wameamua kwenda Nigeria kwa sababu kuna wingi wa walimu na wenye ubora na haikuwa rahisi kuchukua kutoka nchi za jirani kwa sababu na wao pia wana tatizo la uhaba wa waalimu.
”Mchakato wa upatikanaji wa walimu hawa hufanywa kwa kutegemea uwezo wao katika ufundishaji na pia ubora wa kazi zao.” amesema waziri Mjengo
Mkuu wa Wilaya atoa machozi ‘kwa kipigo walichopata Wananchi wake’