China ina baadhi ya majengo na mitambo ya kuvutia zaidi duniani lakini hivi majuzi,ipo klipu ya mgahawa mmoja wa umbo la duara ambayo inaonekana kuwa imejengwa kwenye mabomba ya silinda ya zege ilisambaa sana na kuwashangaza wengi mitandaoni
Video ya mgahawa huo ambao sasa ni maarufu ilichukuliwa katika manispaa ya Chongqing nchini China.
Kulingana na People’s Daily Online, mgahawa huo maarufu wa nyama choma huwapa wateja uzoefu na muonekano wa kipekee kwa kuwapa sehemu kubwa yenye nafasi ilichotengenezwa kwa mabomba ya zege yaliyogeuzwa na kuwa kama chumba private,na wanaweza pia kufurahia muonekano wa jiji kutoka kwenye mgahawa huo.
Kwa kuongezea, watu ambao hawataki kula ndani ya vibanda vya bomba wanaweza kuchagua kuketi kwenye meza zilizowekwa kwenye ua wa mgahawa.