Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ametoa siku tatu kwa Kampuni ya Kufua umeme ya Songas kuhakikisha uzalishaji umeme wa Megawati 180 unarejea kama kawaida badala ya megawati 115 zinazozalishwa sasa.
Aidha, ametoa siku tano kwa kamapuni hiyo kuhakikisha mitambo miwili iliyopo katika matengenezo iwe imekamilika na kufanya kazi.
Dk. Kalemani amebainisha kuwa, masuala ya matengenezo ya mitambo lazima Songas na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakubaliane wakati wa matengenezo na yawe ya kupishanisha ili wasiathiri upatikanaji wa nishati hiyo kwa watanzania.
“Matengenezo yakamilike, sitaki kuona kuna mgao wa umeme, matengenezo yakamilike hali ya umeme irejee kama kawaida” Dk. Kalemani