Baada ya ugunduzi wa gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara wengi wamekuwa wakisubiri namna ambavyo itakuwa na manufaa kwa mwananchi wa kawaida, hapa Ayo Tv imezungumza na mjiolojia kutoka TPDC, Magambo Samweli ambapo ameeleza kiasi cha gesi asilia kilichopo na mpango wa kila mtanzania kupata gesi majumbani na kwenye matumizi ya magari………..
>>> ‘TPDC ina mpango wa kuifanya hii gesi kwa ajili ya matumizi ya magari ambapo vituo takribani 20 vitajengwa kwenye Dar es salaam ambapo wananchi watapata fursa ya kutumia nishati ya gesi kwa matumizi ya magari mpaka sasa hivi kituo kimoja kimejengwa eneo la ubungo’
>>>’Mpaka sasa hivi takribani viwanda 38 mkoa wa Dar es salaam vinatumia gesi na nyumba za shirika la maendeleo la petroli Tanzania wanatumia gesi inayotoka songosongo, mpango uliopo ni kupanua miundombinu ya Dar es salaam kwa kuanzia pamoja na Mtwara na Lindi’
LILIKUPITA HILI JINGINE JIPYA LA GESI ILIYOGUNDULIWA BONDE LA RUVU? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI