Leo July 18, 2019 Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imewaachia huru Askari nane waliokuwa wakikabiliwa na kesi namba 01 ya 2019 ya uhujumu uchumi kwa kutorosha madini ya dhahabu.
Maamuzi hayo yametolewa na Hakimu Mkazi Rhoda Ngimilanga katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza baada ya kusikiliza pendekezo la upande wa mashtaka uliotaka shauri hilo liondolewe Mahakamani na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kwa kuonesha nia ya kutotaka kuendelea na shauri hilo.
Hakimu Rhoda amesema Mahakama imewaondolea mashtaka watuhumiwa hao na wapo huru baada ya DPP kuwasilisha ombi hilo.
Watuhumiwa hao wameachiwa huru kwa mujibu wa kifungu namba 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
LIVE: RAIS MAGUFULI ANAHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA DODOMA
https://www.youtube.com/watch?v=hx2lXJZ5Rug