Mgombea Urais wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa amesema kila Mtanzania atapewa kipande cha heka 1 ya ardhi na kiwanja kimoja cha kuishi bure bila kulipia kodi.
“Hakuna tena kodi ya kiwanja kuanzia tarehe 28 nitakapokuwa Rais, ardhi ni mali ya Wananchi isipokuwa iko chini ya udhamini wa Rais. Hata madini kama yapo kwenye ardhi yako, Mwekezaji akija anakaa na Serikali na anakaa na wewe mnajadili” Mgaywa
Kuhusu utaratibu wa kufanikisha hilo, amesema akishakuwa na Serikali litapelekwa Bungeni na hakuna Mbunge atakataa Sera nzuri kama hiyo.