Moja ya story zilizochukua headlines kutoka Kenya siku ya jana January 05 ilikuwa ni ishu ya mgomo wa walimu wa shule za Serikali wakidai nyongeza ya mshahara.
Taarifa ya Kituo cha Citizen imebaini kuwa wanafunzi wengi walioenda shuleni walilazimika kurudi nyumbani kutokana na kutokuwepo kwa walimu.
Mgomo huu umeanza siku ya kwanza ambapo shule zilikuwa zinafungua baada ya mazungumzo ya Serikali na Chama cha Walimu kutofikia muafaka.
Hapa unaweza kujionea hali ilivyo kupitia taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook